IMEWEKWA SEPTEMBA 11, 2013 SAA 1:17 USIKU
BAADA ya kutua Real Madrid ya Hispania, nyota ya Gareth Bale imeendelea kung'ara, baada ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Wales kupamba kava la mchezo wa kompyuta wa FIFA toleo la 14.
BAADA ya kutua Real Madrid ya Hispania, nyota ya Gareth Bale imeendelea kung'ara, baada ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Wales kupamba kava la mchezo wa kompyuta wa FIFA toleo la 14.
Bale alitua kwa kishindo Bernabeu, na kutambulishwa mbele ya umati kama mchezaji ghali zaidi duniani na kutua kwake kwa Magalactico hao kunahatarisha nafasi ya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji babu kubwa zaidi katika timu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ili kumpa faraja mchezaji mwenzake huyo, alisema mapema kwamba Ronaldo bado mchezaji bora Madrid.
VIDEO Kaangalie tangazo la FIFA 14 linalowahusisha Messi, Bale na wengine...
Nyota wa kava: Gareth Bale na Lionel Messi wamepamba kava la mchezo wa kompyuta wa FIFA 14
Mtu wa Madrid: Gareth Bale ametambulishwa Bernabeu kama mwanasoka ghali zaidi duniani
Lakini katika kuongeza mafuta kwenye moto, Ronaldo ametemwa kwenye kava la mbele la mwaka huu, ambalo limewahusisha Bale na nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Ronaldo na Messi wamekuwa sura ya mechi ya wapinzani wa jadi Hispania, maarufu kama El Classico katika mika ya karibuni, wakiwa wachezaji bora zaidi wawili duniani, lakini Pauni Milioni 86 zilizotolewa kumnunua Bale zinaweza kubadilisha mambo.
Bale alitokea benchi kuichezea Wales usiku wa jana kucheza kwa mara ya kwanza mechi ya ushindani tangu aumie goti na nyonga.
Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham anaweza kuichezea Madrid kwa mara ya kwanza dhidi ya Villarreal Jumamosi.
Lakini mechi yake ya kwanza anaweza kucheza beki ya kushoto, baada ya wote Marcelo na Fabio Coentrao kuwa majeruhi wakicheza mechi za kimataifa.
Namba moja? Hakukuwa na nafasi ya Cristiano Ronaldo katika kava la mwaka huu la FIFA 14
Bora duniani? Lionel Messi ni moja ya sura zilizomo katika mchezo mpya wa kompyuta wa FIFA 14