• HABARI MPYA

    Wednesday, September 11, 2013

    BALAA ARSENAL, YAYA AUMIA NA SASA WENGER ABAKI NA MSHAMBULIAJI MMOJA TU ALIYE FITI

    IMEWEKWA SEPTEMBA 11, 2013 SAA 6:19 MCHANA
    UHABA wa washambuliaji umeongezeka kwa Arsene Wenger, baada ya Yaya Sanogo kuumia na kuifanya Arsenal sasa ibaki na mshambuliaji mmoja tu wa kati aliye fiti.
    Sanogo - ambaye kwa sasa ni mshambuliaji chaguo la pili Arsenal- amerejea katika klabu hiyo kutoka kuichezea timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21 akiwa majeruhi.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atafanyiwa matibabu makini makao makuu ya klabu, Colney, London kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa mwishoni mwa wiki na Sunderland - ambao utakuwa wa kwanza pia kwa mchezaji mpya ghali wa klabu hiyo, Mesut Ozil aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42 kutoka real Madrid. debut.
    Blow: Yaya Sanogo injured himself on international duty with the France Under 21's
    Pigo: Yaya Sanogo ameumia akicheza Ufaransa U21
    Pressure: Olivier Giroud is now the only fit, recognised striker at the club
    Presha: Olivier Giroud sasa ndiye mshambulaji pekee wa kati aliye fiti katika klabu hiyo

    Majeruhi hayo yanamaanisha, Olivier Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kati aliye fiti katika klabu hiyo kuelekea mchezo wa Jumamosi Uwanja wa Light.
    Sanogo, aliyesajiliwa kutoka Auxerre majira haya ya joto, alisajiliwa na Wenger kwa ajili ya kuandaliwa aje kuisaidia klabu baadaye, lakini uhaba wa washambuliaji umefanya apewe majukumu mapema kikosi cha kwanza.
    Klabu hiyo ilikwama kuwasajili Luis Suarez, Gonzalo Higuain, Wayne Rooney, Karim Benzema na Demba Ba hivyo kumuachia wakati mgumu Wenger.
    Lukas Podolski anaweza kucheza badala ya Giroud, lakini naye anatakiwa kuwa nje kwa miezi mitatu sababu ya maumivu ya nyama, wakati Nicklas Bendtner - ambaye klabu ilijaribu kumuuza wakati wa dirisha la usajili, hayuko fiti kwa mechi.
    Chance: Sanogo barely had a chance to impress Arsene Wenger before the injury
    Nafasi: Sanogo alipewa nafasi ya kufanya vitu kwenye kikosi cha Arsene Wenger kabla ya kuumia
    Record breaker: Mesut Ozil was Arsenal's only major signing this summer
    Mvunja rekodi: Mesut Ozil ndiye mchezaji pekee mkubwa aliyesajiliwa na Arsenal msimu huu

    Mbali ya Sanogo, Wenger anaweza kuwatumia Theo Walcott katikati, wakati kidna wa miaka 17, Chuba Akpom anaweza kuanzia benchi.
    Habari njema kwa Wenger ni kurejea kwa Thomas Vermaelen kuanza mazoezi kamili. Nahodha huyo wa klabu, amekuwa nje mwanzoni mwa msimu kwa sababu ya maumivu, lakini alianza mazoezi mepesi mwishoni mwa mwezi uliopita.
    Lakini Vermaelen ameanza mazoezi kamili na bila shaka anarejea kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Wenger.
    Returning to full training: Thomas Vermaelen is set to give Arsenal a much-needed fitness boost
    Ameanza mazoezi kamili: Thomas Vermaelen anatarajiwa kuongeza nguvu Arsenal
    Favourite position: Theo Walcott has been tried up-front in the past
    Nafasi adimu: Theo Walcott amejaribu kucheza katikati siku za nyuma
    Worries: Lukas Podolski is injured while Nicklas Bendtner is severely unfit
    Worries: Lukas Podolski (left) is injured while Nicklas Bendtner (right) is severely unfit
    Hakuna namna: Lukas Podolski (kushoto) ni majeruhi wakati Nicklas Bendtner (kulia) haamini tena
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BALAA ARSENAL, YAYA AUMIA NA SASA WENGER ABAKI NA MSHAMBULIAJI MMOJA TU ALIYE FITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top