Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 11, 2013 SAA 5:47 ASUBUHI
KIUNGO wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa ‘Babu’ amefiwa na mama yake mzazi, Bi Joha leo mjini Mwanza na mazishi yanatarajiwa kufanyika jioni ya leo mjini humo.
Kwa sababu hiyo, mtoto wa mchezaji huyo wa zamani wa Pamba SC pia ya Mwanza, Mrisho anayechezea Yanga SC naye amepanda ndege leo kwenda Mwanza kumzika bibi yake aliyefariki akiwa na umri wa miaka 102.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Mrisho amesema kufuatia msiba wa bibi yake mzaa baba, sasa hatakwenda na timu yake, Yanga SC Mbeya badala yake anakwenda kuzika kwanza Mwanza.
Mrisho alisema kwamba baada ya mazishi leo, kesho atapanda ndege kwenda kuungana na wenzake Mbeya.
Hata hivyo, Ngassa kwa sasa hachezi kutokana na kuwa bado anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi sita na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kusaini timu mbili, Simba na Yanga SC. Tayari amekosa mechi tatu.
Ngassa ametakiwa arejeshe fedha za Simba SC Sh. Milioni 30 na kulipa fidia ya Sh. Milioni 15 ndipo aruhusiwe kuchezea Yanga SC.
Tayari kikosi cha Yanga kipo njiani na basi lao kwenda Mbeya kwa ajili ya michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Jumamosi dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine mjini humo na Jumatano dhidi ya Prisons.

![]() |
| Pole Babu; Khalfan Ngassa kulia amefiwa na mama yake mzazi |
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Mrisho amesema kufuatia msiba wa bibi yake mzaa baba, sasa hatakwenda na timu yake, Yanga SC Mbeya badala yake anakwenda kuzika kwanza Mwanza.
![]() |
| Pole kwa msiba wa bibi; Mrisho Ngassa akiwa na mabosi wa Yanga SC, kulia Francis Kifukwe na kushoto Mussa Katabaro |
Mrisho alisema kwamba baada ya mazishi leo, kesho atapanda ndege kwenda kuungana na wenzake Mbeya.
Hata hivyo, Ngassa kwa sasa hachezi kutokana na kuwa bado anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi sita na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kusaini timu mbili, Simba na Yanga SC. Tayari amekosa mechi tatu.
Ngassa ametakiwa arejeshe fedha za Simba SC Sh. Milioni 30 na kulipa fidia ya Sh. Milioni 15 ndipo aruhusiwe kuchezea Yanga SC.
![]() |
| Pumzika kwa amani; Bibi Joha enzi za uhai wake. Mungu amuweke pema peponi. Amin. |

.png)