• HABARI MPYA

    Thursday, October 03, 2013

    AMIR KHAN KUZIPIGA NA MAYWEATHER MEI 3 LAS VEGAS

    IMEWEKWA OKTOBA 3, 2013 SAA 6:59 USIKU
    BONDIA Amir Khan anatarajiwa kuzipiga na Floyd Mayweather katika pambano la 'utajiri' zaidi kuwahi kumuhusisha bondia wa Uingereza.
    Mbabe huyo Bolton na shukaa wa zamani wa Olimpiki atakutana na bondia mkali wa kutupa makonde duniani mjini Las Vegas, Mei 3, mwakani.
    Katika pambano hilo litakalokuwa na thamani ya Pauni Milioni 200, Khan anaweza kulipwa si chini ya Pauni Milioni 6 na anaweza kupata jumla ya mara mbili ya kiasi hicho cha fedha kutokana na malipo ya haki za Televisheni.
    Champion: Floyd Mayweather poses with Justin Bieber after beating Canelo Alvarez in Las Vegas
    Bingwa: Floyd Mayweather akiwa katika picha ya pamoja na Justin Bieber baada ya kumpiga Canelo Alvarez mjini Las Vegas
    Down and out: Amir Khan was put on the canvas by Julio Diaz in his last fight
    Chini na nje: Amir Khan alipigwas na Julio Diaz katika pambano lake la mwisho

    HUYU NA YULE...

    KHAN
    MAYWEATHER
    26UMRI36
    Bolton, UKKUZALIWAGrand Rapids, US
    King KhanJINA A UTANIMoney
    OrthodoxSTAILIOrthodox
    5ft 9inUREFU5ft 8in
    7inUPANA72in
    31MAPAMBANO45
    28 (19)KUSHINDA (KO)45 (26)
    3 (2)KUPIGWA (KO)0 (0)
    Tangazo rasmi la pambano hilo linatarajiwa kutolewa musa si mrefu tangu sasa na Khan tayari amejitoa kwenye pambano la ubingwa wa dunia uzito wa Welter dhidi ya Devon Alexander, lililokuwa lifanyike Desemba 7 mjini New York, ili kutimiza ndoto zake za kupigana na Mayweather.
    Khan amepata nafasi hiyo pekee maishani mwake kutokana na kasi yake ya upiganaji ulingoni inayoaminika itampa changamoto nzuri Mayweather.
    Khan tayari ameanza maandalizi Jijini California kwa ajili ya pambano na Alexander na atabakia huko moja kwa moja na kocha wake mpya, Virgil Hunter kwa miezi mingine saba akiendelea na maandalizi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AMIR KHAN KUZIPIGA NA MAYWEATHER MEI 3 LAS VEGAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top