IMEWEKWA OKTOBA 5, 2013 SAA 2:30 USIKU
Ndugu wahariri, waandishi wa habari na watangazaji wa redio na televisheni
Kwanza nachukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru kwa kuitikia mwaliko wetu na kuja hapa leo hii kwenye semina hii fupi ya kutambulisha kwenu kampeni mpya ya Kilimanjaro Premium Lager itakayojulikana kama NANI MTANI JEMBE.
Kama mnavyojua Kilimanjaro Premium Lager imekuwa mdhamini mkuu wa Simba na Yanga kwa miaka mitano sasa tangu mwaka 2008 ambapo tulisaini mkataba kwa mara ya kwanza na kuongeza tena mkataba wa miaka mitano mwaka 2011 ambao utadumu mpaka mwaka 2016.
Lengo letu kubwa katika udhamini huu ni kuziimarisha Simba na Yanga ili ziendelee kuwa fahari ya Watanzania kama ilivyo bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Vilevile udhamini huu ulilenga kuitangaza bia ya Kilimanjaro Premium Lager kupitia klabu hizi kongwe zenye historia kubwa katika taifa hili.
Naamini kwamba Watanzania tumegawanyika mara mbili. Bila kujali dini wala kabila, kila Mtanzania aidha ni shabiki wa Simba au Yanga nah ii ni kutokana na historia kubwa ambayo vilabu hivi vimeijenga na pia kutokana na sifa kubwa ambayo vilabu hivi vimeiletea Tanzania katika bara letu la Afrika kutokana na utani wa jadi ambao ni mojawapo ya mambo yanayotutambulisha Watanzania. Utani huu wa jadi umekuwa chachu kubwa ya maendeleo ya vilabu hivi kwa sababu unaleta msukumo wa kila klabu kuhakikisha inajiimarisha ili kushindana ipasavyo na kupata mafanikio. Vile vile utani huu wa jadi umeweza kuleta msisimko wa aina yake kati ya mashabiki. Lengo letu la kuwaalika hapa siku ya leo ni kuhakikisha kuwa nyie kama wanahabari mnaelewa vizuri kuhusu NANI MTANI JEMBE ili muweze kuwaelimisha wale wote ambao hawakupata fursa ya kuja hapa na wale wote wanaosikiliza redio na televisheni zenu pamoja na kusoma blogu zenu na magazeti yenu.
Kupitia kampeni ya NANI MTANI JEMBE, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeamua kutumia utani huu wa jadi uliopo kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kuendelea kuwaleta pamoja mashabiki. NANI MTANI JEMBE itazinduliwa kesho tarehe 6 Oktoba, 2013 kwenye viwanja vya Leaders Club na itadumu kwa siku 75 kuanzia mpaka Desemba 14 2013.
Kama nilivyosema awali, NANI MTANI JEMBE itahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga.
• Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
• Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni 50.
• Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh. 1,000.
• Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
• Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua kulingana upigaji kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
Nyinyi kama mashabiki wa Simba na Yanga na vile vilevile waandishi wa habari tunaomba mtusaidie kueneza ujumbe huu wa Nani Mtani Jembe.
Kampeni ya Nani Mtani Jembe itawafikia mashabiki wote wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia matukio mbalimbali yatakayofanyika nchi nzima na matukio hayo ni pamoja na :
Bar promotions, Road shows, Mabonanza ya kila wiki, Mashindano ya Fussball (mpira wa mezani) na mambo mengine mengi ya kusisimua.
Mashabiki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali zitakazotolewa kupitia matukio haya na vilevile mashabiki watakaopiga kura wataweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku zitakazokuwa kwenye vizibo vya chupa za Kilimanjaro Premium Lager.
Nyinyi kama watani wa jadi mnaozipenda klabu zenu tunawaomba muwe mabalozi wa kampeni hii ili mwishoni tuone NANI MTANI JEMBE.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Ndugu wahariri, waandishi wa habari na watangazaji wa redio na televisheni
Kwanza nachukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru kwa kuitikia mwaliko wetu na kuja hapa leo hii kwenye semina hii fupi ya kutambulisha kwenu kampeni mpya ya Kilimanjaro Premium Lager itakayojulikana kama NANI MTANI JEMBE.
Kama mnavyojua Kilimanjaro Premium Lager imekuwa mdhamini mkuu wa Simba na Yanga kwa miaka mitano sasa tangu mwaka 2008 ambapo tulisaini mkataba kwa mara ya kwanza na kuongeza tena mkataba wa miaka mitano mwaka 2011 ambao utadumu mpaka mwaka 2016.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kaishe itoa semina |
Waandishi wa Habari wakisikiliza |
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akitoa semina |