IMEWEKWA OKTOBA 4, 2013 SAA 5:08 USIKU
KUNA wakati majira ya joto mashabiki wa Liverpool walikuwa wana wasiwasi Luis Suarez hatakuwamo katika kikosi chao tena. Lakini mshambuliaji huyo mtata ameungana na wachezaji wenzake Ijumaa ya leo mchana kwa ajili ya picha ya kikosi cha msimu huu.
Akitoka kufunga bao dhidi ya Sunderland katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya England tangu amng'ate beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic na kufungiwa mechi 10, Suarez kuweza kutabasamu akiwa ameketi jirani na Philippe Coutinho na Jordan Henderson.
Liverpool imekuwa katika mwanzo mzuri kwenye Ligi Kuu ikivuna pointi 13 katika mechi zao sita za mwanzoni na Suarez hakuwa mshambuliaji pekee aliye katoa fomu aliyeshiriki picha hiyo, bali hata Daniel Sturridge pia alikuwepo.
KIKOSI CHA LIVERPOOL 2013-14
NYUMA (Kutoka kushoto) Graham Carter (Kit Coordinator), Ryland Morgans (Mkuu wa mazoezi ya viungo), Chris Davies (Mkuu wa uchambuzi wa wapinzani), John Achterberg (Kocha wa makipa), Chris Morgan (Mtaalamu wa viungo), Andre Wisdom, Martin Kelly, Brad Jones, Simon Mignolet, Tiago Ilori, Victor Moses, Glen Driscoll (Mkuu wa uchezaji), Jordan Milsom (Kocha wa mazoezi ya nguvu na Rehab), Matt Konopinski (Mtaalamu wa viungo), Lee Radcliffe (Meneja vifaa), Ray Haughan (Meneja Utawala wa timu).
KATIKATI (Kutoka kushoto) Harrison Kingston (Mchambuzi wa kikosi cha kwanza), Paulo Barreira (Mtaalamu wa viungo), Dk Zaf Iqbal (Mkuu wa Dawa), Colin Pascoe (Kocha Msaidizi), Raheem Sterling, Iago Aspas, Luis Alberto, Mamadou Sakho, Sebastian Coates, Aly Cissokho, Jordan Ibe, Jonathan Flanagan, Mike Marsh (Kocha wa kikosi cha kwanza), Paul Small (Mchua misuli), Sylvan Richardson (Mchua misuli), Pedro Philippou (Daktari wa michezo).
MBELE (Kutoka kushoto) Philippe Coutinho, Luis Suarez, Jordan Henderson, Glen Johnson, Martin Skrtel, Steven Gerrard (Nahodha), Brendan Rodgers (Kocha), Daniel Agger, (Nahodha Msaidizi), Jose Enrique, Daniel Sturridge, Lucas Leiva, Kolo Toure na Joe Allen.
Na nani anaweza kumlamu? Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Manchester City anaongoza chati ya ufungaji Ligi Kuu ya England baada ya kufunga mabao matano hadi sasa. Pia alifunga mabao mawili katika ushindi wa Liverpool wa 4-2 kwenye Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One dhidi ya Notts County.
Sturridge, ambaye anatarajiwa kuichezea England katika michezo ya wiki ijayo kuwania tiketi ya Kombe la Dunia dhidi ya Poland na Montenegro, ataungana na wachezaji wenzake wa kimataifa, akiwemo Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, baada ya mechi na Crystal Palace Jumamosi.
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard akiwa na wachezaji wenzake mazoezini Melwood leo mchana
Suarez akionekana mwenye furaha mazoezini