IMEWEKWA OKTOBA 5, 2013 SAA 12:09 ASUBUHI
KOCHA Jose Mourinho amesema hajutii kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Romelu Lukaku kwenda Everton.
Kocha huyo Chelsea alimshuhudia Lukaku akifunga mabao mawili dhidi ya Newcastle Jumatatu, akiongezea kwenye bao lake la kwanza alilofunga dhidi ya West Ham.
Pamoja na kufunga mabao hayo matatu, lakini Mourinho amesema timu yake ni tofauti sana na ya Roberto Martinez.
Macho makini: Jose Mourinho alimshuhudia mshambuliaji aliemtoa kwa mkopo Romelu Lukaku akicheza vizuri Everton
Kwa penalti: Lukaku aliifungia mabao mawili Toffees dhidi ya Newcastle Jumatatu
Chelsea itakwenda kucheza na Norwich kesho, na Mourinho anatarajiwa kushusha kikosi kikali kilichoifunga Steaua mabao 4-0 mjini Bucharest Jumanne.
Alipoulizwa kama anajuta kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo, Mourinho alisema: "Hapana. NI kitu kimoja kuchezea Everton, na kingine kuchezea Chelsea,".