• HABARI MPYA

    Friday, October 04, 2013

    TUZO ZA WANAMICHEZO BORA ZA TASWA SASA LABDA DESEMBA 20

    Na Mwandishi Wetu, IMEWEKWA OKTOBA 4, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
    CHAMA cha Waandishi wa Habari  za Michezo Tanzania (TASWA), kimesema kwamba Tuzo ya Wanamichezo Bora wa mwaka 2012 zitafanyika Desemba 20 mwaka huu, katika ukumbi ambao utatajwa baaaye.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo, Hajji Manara amewaambia Waandishi wa Habari leo kwamba, wamefanya vikao kadhaa cha mwisho kikiwa jana kati ya Kamati ya Utendaji ya TASWA na Kamati ya Tuzo, kutafakari athari za kuchelewa kufanya na zile za kuacha kufanya, wakajiridhisha ni bora kufanya ingawa wamechelewa, ili kuwaenzi wanamichezo waliofanya vizuri mwaka uliopita.
    Ataibuka? Salum Abubakar 'Sure Boy' aling'ara msimu uliopita, je atang'ara katika tuzo za TASWA mwaka huu?

    “Tunaomba radhi wanamichezo wanaowania tuzo hizo, vyama mbalimbali vya michezo na wote ambao kwa namna moja au nyingine kuchelewa kwetu kuliwakwaza, lakini hatukuwa na jinsi yote ni katika kuhakikisha tuzo zetu zinakuwa bora kama miaka iliyopita,”alisema mtoto huyo wa mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Sunday Manara.
    Hajji alisema majina ya awali ya wanaowania tuzo kwa michezo mbalimbali tayari yalikwishatangazwa, na sasa ni jukumu sasa la Kamati ya Tuzo kuendelea na mchakato ili kuhakikisha zinakuwa nzuri zaidi.
    Alisema tuzo hizo zimechelewa kufanyika kutokana na sababu mbalimbali, ambazo zipo nje ya uwezo wa Kamati yake, Kamati ya Utendaji ya TASWA, wanachama wa TASWA, wanamichezo husika na wandishi wa habari za michezo kwa ujumla wao.
    “Ninyi ni mashahidi wa tuzo za miaka miwili iliyopita, zilivyofana na zikabaki kupigiwa mfano kwa ubora wake. Lakini mwaka huu, mambo kidogo yalikuwa magumu kutokana na kampuni ambayo sitaitaja jina, ambayo awali ilituhakikishia ingedhamini  kwa asilimia 100 lakini ilipata matatizo ya kiuchumi wiki tatu kabla ya tarehe tuliyokuwa tumepanga kufanya tuzo, hivyo wakatuomba tusogeze mbele huenda mambo yangeimarika,”.
    “Kuanzia hapo kila mara wakawa wanatuhakikishia mambo yatakuwa mazuri, lakini mwezi Agosti mwishoni wakatupa taarifa rasmi kuwa hawatamudu kudhamini tuzo zetu, hali ambayo ilituchanganya kwa kiasi kikubwa kwani ingekuwa vigumu sana kupata wadhamini wa ghafla kwa wakati huo,”.
    “Hata hivyo kutokana na heshima ambayo TASWA imejijengea na kuaminika mbele ya jamii kwa kushirikiana na Kamati ya Tuzo, tukaanza mazungumzo na kampuni mbalimbali na tayari tumepata kampuni mbili za kutusaidia, huku tukiendelea na juhudi zetu za kupata wadhamini wa kutosha kulingana na bajeti yetu,”alisema Haji Manara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TUZO ZA WANAMICHEZO BORA ZA TASWA SASA LABDA DESEMBA 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top