• HABARI MPYA

    Wednesday, November 20, 2013

    AZAM FC WAITANDIKA YANGA 2-0 CHAMAZI, MTIBWA SUGAR, ASHANTI NAZO ZANG’ARA

    Na Prince Akbar, Chamazi
    AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya timu za vijana za klabu za Ligi Kuu ya Bara chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la Uhai, baada ya kuilaza mabao 2-0 Yanga SC, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
    Mabao ya Azam leo yamefungwa na Adam Omar dakika ya saba na Gadiel Michael dakika ya 39.
    Katika mchezo mwingine uliofanyika Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam jioni hii, bao pekee la Patrick Mdidi dakika ya 38 limetosha kuipa Mtibwa Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora.

    Katika mechi za asubuhi, Ashanti United iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha Uwanja wa Azam Complex. Mabao yote ya Ashanti yalifungwa na mtoto wa beki wa zamani wa kimataifa Tanzania na klabu ya Yanga, Salum Kabunda ‘Ninja Msudan’ (marehemu), aitwaye Ally Salum Kabunda anayecheza na mdogo wake, Hassan Salum Kabunda pia katika timu hiyo na wote wafungaji wazuri.
    Uwanja wa Karume, Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons ya Mbeya, mabao ya Mohammed Mohammed na Hassan Rajab, wakati Uwanja wa DUCE, Mbeya City iliifunga 1-0 JKT Ruvu na Ruvu Shooting ikatoka sare ya 1-1 na Mgambo JKT.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WAITANDIKA YANGA 2-0 CHAMAZI, MTIBWA SUGAR, ASHANTI NAZO ZANG’ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top