• HABARI MPYA

    Wednesday, November 20, 2013

    HIZI NI DALILI TUZO YA MWANSOKA BORA WA DUNIA SASA YA RONALDO? FIFA YASOGEZA MBELE UPIGAJI KURA BALLON D'OR

    KATIKA usiku ambao Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu matamu, hat-trick iliyoipeleka Ureno Fainali zijazo za Kombe la Dunia mwakani, FIFA imeongeza muda wa kupiga kura za kuchagua mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d’Or. 
    Zoezi la upigaji kura lilifungwa Novemba 15, lakini Manahodha, Makocha Vyombo vya Habari ambavyo hazijawasilisha kura zao, wamepewa siku tisa zaidi kuwasilisha orodha zao za wachezaji watatu wa kwanza.
    FIFA, ambayo imethibitisha uamuzi wake leo asubuhi, pia imethibitisha kwamba wale ambao tayari wamekwishapiga kura wanaweza kurekebisha majina yao na kuwasilisha tena.
    Shujaa wa mechi: Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick dhidi ya Sweden kuipeleka Ureno Brazil
    Lionel Messi
    Franck Ribery
    Washindani: Nyota wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) amekwishashinda tuzo nne za Ballon d'Or na Franck Ribery wa Ufaransa na Bayern Munich (kulia) anapewa nafasi ya kufanya vizuri baada ya kushinda mataji matatu akiwa Bayern Munich.
    Yaya Toure
    Robin van Persie
    Wawakilishi wa Ligi Kuu England: Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (kushoto) na mshambuliaji wa Man United, Robin van Persie (kulia)

    Ronaldo jana usiku ameifungia Ureno mao matatu peke yake ikishinda 3-2 dhidi ya Sweden na kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani Brazil.
    Ureno inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mao 4-2 baada ya awali kushinda 1-0 wiki iliyopita nyumbani, bao pekee la Ronaldo. Zlatan Ibrahimovic alijitahidi kuisaidia timu yake jana na akafunga mabao mawili, lakini bahati haikuwa yao.
    Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika za 50, 77 na 79, wakati  Ibrahimovic alifunga dakika ya 68 na 72.

    ORODHA KAMILI YA WACHEZAJI 23 WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA WA BORA WA DUNIA...

    Gareth Bale (Wales/Real Madrid)
    Edinson Cavani (Uruguay/PSG)
    Cristiano Ronaldo (Ureno/Real Madrid)
    Radamel Falcao (Colombia/Monaco)
    Eden Hazard (Ubelgiji/Chelsea)
    Zlatan Ibrahimovic (Sweden/PSG)
    Andres Iniesta (Hispania/Barcelona)
    Philipp Lahm (Ujerumani/Bayern Munich)
    Robert Lewandowski (Poland/Dortmund)
    Lionel Messi (Argentina/Barcelona)
    Thomas Muller (Ujerumani/Bayern Munich)
    Manuel Neuer (Ujerumani/Bayern Munich)
    Neymar (Brazil/Barcelona)
    Mesut Ozil (Ujerumani/Arsenal)
    Andrea Pirlo (Italia/Juventus)
    Franck Ribery (Ufaransa/Bayern Munich)
    Arjen Robben (Uholanzi/Bayern Munich)
    Bastian Schweinsteiger (Ujerumani/Bayern Munich)
    Luis Suarez (Uruguay/Liverpool)
    Thiago Silva (Brazil/PSG)
    Yaya Toure (Ivory Coast/Manchester City)
    Robin van Persie (Uholanzi/Manchester United)
    Xavi (Hispania/Barcelona)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HIZI NI DALILI TUZO YA MWANSOKA BORA WA DUNIA SASA YA RONALDO? FIFA YASOGEZA MBELE UPIGAJI KURA BALLON D'OR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top