KIUNGO asiyetakiwa Manchester United, Anderson ametua Florence tayari kwa vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na Fiorentina katika Ligi ya Serie A.
Mbrazil huyo amewaambia rafiki zake anataka uhamisho wa moja kwa moja kujihakikishia namba, lakini United wanataka kumtoa kwa mkopo tu kwa wakati huu.
Anderson aliondoka Frankfurt leo asubuhi – alipotua akitokea Manchester kuunganisha ndege– na dili la mkopo linatarajiwa kukamilishwa mchana wa kesho.
0 comments:
Post a Comment