Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
TIMU za Uganda, URA na KCC zimefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi jioni hii baada ya ushindi dhidi ya wapinzani wao KMKM na Tusker katika mechi za Robo Fainali.
URA imeifunga 1-0 KMKM ya Zanzibar, bao pekee la Owen Kasuule dakika ya 42 Uwanja wa Gombani, Pemba wakati KCC imeitoa kwa penalti 4-3 Tusker kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kipa wa KCC, Omar Magoola alipangua penalti mbili za Ismail Dunga na Luke Ochieng, wakati za Clifford Alwanga, Brian Osumba na kipa mwenzake Samuel Odhiambo zilimpita.
Waliofunga penalti za KCC ni Tony Odur, Habib Kavuma, Stephen Bengo na kipa Omar Magoola na kwa matokeo hayo, Tusker itamenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza keshokutwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar Saa 10:00 jioni.
Robo Fainali ya mwisho itachezwa Saa 2:00 usiku Uwanja wa Amaan kati ya Simba SC na Chuoni na mshindi atakutana na URA katika Nusu Fainali ya pili keshokutwa Saa 2:00 Usiku.
Wakati huo huo, mchezaji Stephen Bengo amezawadiwa king’amuzi cha Azam TV baada ya kuwa mchezaji bora wa mechi kati ya KCC na Tusker.
Uwanja wa Gombani, Pemba Mohamed Mtwango wa Cloves Stars alizawadiwa king’amuzi hicho pia baada ya kuwa mchezaji wa mechi dhidi ya Azam na

![]() |
KCC imefuzu Nusu Fainali |

0 comments:
Post a Comment