• HABARI MPYA

    Wednesday, January 08, 2014

    AZAM WA KWANZA KUTINGA NUSU FAINALI MAPINDUZI

    Na Mwandishi Wetu, Pemba
    AZAM FC imekuwa timu ya kwanza kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya mchana wa leo kuilaza mabao 2-0 Cloves Stars Uwanja wa Gombani Pemba.
    Mabao yaliyoipeleka Azam Nusu Fainali yamefungwa na mabeki Aggrey Morris dakika ya 68 na Waziri Salum dakika ya 85.
    Aggrey alifunga bao lake kwa guu lake la kulia baada ya kuuwahi mpira uliorudi kufuatia yeye mwenyewe kuunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Malika Ndeule.
    Azam inatisha

    Waziri naye alifunga bao lake baada ya kupokea pasi maridadi ya ‘kiungo kweli’ Ibrahim Mwaipopo akiwa ndani ya sita na kumchambua vizuri kipa wa Karafuu.
    Azam sasa inasubiri mshindi kati ya Tusker FC ya Kenya na KCC ya Uganda mechi inayoendelea Uwanja wa Amaan, Zanzibar ikutane naye katika Nusu Fainali. Robo Fainali nyingine inayoendelea hivi sasa ni kati ya KMKM na URA ya Uganda, Uwanja wa Gombani, wakati usiku Simba SC itamenyana na Chuoni.
    Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ali, Malika Ndeule/Saleh Abdallah, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Farid Mussa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Umony/Muamad Kone, Kipre Tchetche/Seif Abdallah na Khamis Mcha ‘Vialli’/Ibrahim Mwaipopo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM WA KWANZA KUTINGA NUSU FAINALI MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top