• HABARI MPYA

    Friday, January 17, 2014

    COASTAL ‘WABEBA’ TAJI LA KWANZA BAADA YA MIAKA 26

    Na Mahmoud Zubeiry, Muscat
    MARA ya mwisho Coastal Union ya Tanga kushinda taji ilikuwa ni mwaka 1988 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
    Tangu wamekabidhiwa Kombe la ubingwa wa Bara, Coastal hawajawahi kukabidhiwa taji lingine kwa sababu hawajashinda mashindano yoyote mengine baada ya hapo.

    Mwenyekiti wa Fanja, Saif Al Sumry kushoto akimkabidhi Ngao Mwenyekiti wa Coastal Union, Hilal Hemed 'Aurora' baada ya mchezo wa jana. Wegine wanaoshuhudia ni Makamu Mwenyekiti wa Fanja kushoto, Ahmed Al  Busaidy, Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania hapa Oman, Said Mussa na Meneja wa Coastal, Akida kulia
    Lakini jana, ikiwa ni miaka 26 baadaye, timu hiyo ilipewa taji, baada ya kukabidhiwa Ngao ya Urafiki na klabu ya 
    Fanja ya Oman, kutokana na kuzuru nchini hapa kucheza mechi ya kirafiki na klabu hiyo kigogo hapa.
    Mwenyekiti wa Coastal, Hilal Hemed ‘Aurora’ alikuwa mwenye tabasamu pana wakati anapokea Ngao hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Fanja, Saif Al Sumry.  Mataji matamu, lakini lazima wayapiganie uwanjani.
    Kiungo wa Coastal Union ya Tangam Jerry Santo akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Fanja ya Oman jana katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Fanja, Muscat, Oman, Fanja ilishinda 1-0.
    Razack Khalfan nyuma akimdhibiti kiungo wa Fanja
    Mshambuliaji wa Coastal akikabiliana na mchezaji wa Fanja
    Hatari kwenye lango la Fanja
    Haruna Moshi 'Boban' wa Coastal hapa alimpiga chenga moja hatari sana mchezaji huyu wa Fanja, kweli ujuzi hauzeeki
    Wachezaji wa Fanja na Coastal wakigombea mpira
    Jerry Santo kulia akimburuza kiungo wa Fanja
    Wachezaji wa Coastal na baridi la Oman hadi kujifunika mablanketi benchi
    Wachezaji, viongozzi na makocha wa Fanja na Coastal katika picha ya pamoja kabla ya mechi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL ‘WABEBA’ TAJI LA KWANZA BAADA YA MIAKA 26 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top