MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Neymar ameumia kifundo cha mguu akiichezea timu yake mechi ya Copa del Rey ikishinda 2-0 jana dhidi ya Getafe katika mechi ya Kombe la Mfalme.
Sasa Mbrazil huyo anaweza kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City mwezi ujao.
Lionel Messi alifunga mabao yote katika mechi hiyo ya marudiano ya 16 Bora na kufanya ushindi wa jumla wa 6-0.
Barça itasafiri hadi Etihad Februari 18 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa na Mbrazil, Neymar huenda akawa bado anauguza maumivu ya kifundo cha mguu wa kulia.
![]() |
Messi alifunga mabao yote mawili ya Barca jana Kombe la Mfalme |
Maumivu: Neymar alivyoumia jana na kutolewa nje
Neymar akiondolewa uwanjani na madaktari wa timu
Neymar aliumia baada ya kupewa pigo na beki wa Getafe, Alexis Ruano
0 comments:
Post a Comment