• HABARI MPYA

    Sunday, January 05, 2014

    STEPHEN BENGO AIPELEKA ROBO FAINALI KCC KOMBE LA MAPINDUZI, AFC LEOPARD NJE

    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    AFC Leopard ya Kenya, imeaga michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa mabao 3-0 na KCC ya Uganda katika mchezo wa Kundi B jioni hii Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    KCC inapanda kileleni mwa Kundi B baada ya kumaliza na pointi saba na ili kubaki hapo, itategemea na matokeo ya mchezo wa pili kati ya Simba SC na KMKM.
    Kifaa; Stephen Bengo ameendelea kung'ara Kombe la Mapinduzi Zanzibar

    Mabao yaliyoizamisha Leopard hii leo yamefungwa na Herman Wasswa dakika ya 30, Stephen Bengo aliyewahi kuchezea Yanga SC, dakika ya 71 na Masiko Tom dakika ya 79.
    Leopard baada ya kufungwa 1-0 na Simba SC katika mchezo wa kwanza, ilimpandisha ndege mshambuliaji wake hatari, Alan Wanga kutoka Nairobi kuja Zanzibar kuongeza nguvu.
    Na baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na KMKM juzi, ikampandisha ndege beki wake, hodari James Situma kuja kuongeza nguvu- lakini wote wameshindwa kuisaidia timu hiyo na sasa inarejea Kenya baada ya hatua ya makundi tu.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STEPHEN BENGO AIPELEKA ROBO FAINALI KCC KOMBE LA MAPINDUZI, AFC LEOPARD NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top