| Kiungo Athumani Iddi 'Chuji' (kulia) aliibuka Uwanja wa Taifa jioni ya leo baada ya mechi ya timu yake Yanga SC dhidi ya Mbeya City kuwapongeza wachezaji wenzake kwa ushindi wa 1-0. Chuji alikuwa mwenye furaha sana na aliwapungia mkono mashabiki kuwapa ishara ya kuomba msamaha, kufuatia kusimamishwa kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa tuhuma za utovu wa nidhamu. Mashabiki walimfurahia sana mtaalamu huyo wa pasi 'zenye macho' alipotokea Taifa. Kushoto ni beki Rajab Zahir. |
0 comments:
Post a Comment