KILA LA HERI AZAM FC, YAWANIA KUSONGA MBELE AFRIKA LEO DHIDI YA WAMAKONDE UGENINI
Azam FC leo inamenyana na wenyeji Ferroviario mjini Beira katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika, ikihitaji sare tu ili kusonga mbele baada ya wiki iliyopita kushinda bao 1-0 mjini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Azam FC,Nassor Idrisa 'Father' wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea mchezo huo na wana matumaini ya kufuzu mtihani huo mgumu. Kila la heri Azam FC ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment