• HABARI MPYA

    Saturday, April 12, 2014

    JKT RUVU YAIPIGA 1-0 COASTAL MKWAKWANI

    Na Oscar Assenga, Tanga
    BAO pekee la Gido Chawala limeipa JKT Ruvu ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani jioni hii mjini humo.
    Chawala alifunga bao hilo kwa penalti, baada ya kiungo wa Coastal, Suleiman Kassim ‘Selembe’ kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

    Matokeo hayo yanaifanya JKT Ruvu inayofundishwa na Freddy Felix Isaya Kataraiya Minziro ‘Majeshi’ itimize pointi 31 baada ya kucheza mechi 25 na kujiweka salama kabisa katika Ligi Kuu, ikiwa nafasi ya saba.
    Coastal Union yenyewe inabaki na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 25 na inabaki pia nafasi ya tisa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT RUVU YAIPIGA 1-0 COASTAL MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top