• HABARI MPYA

    Tuesday, July 15, 2014

    DIEGO COSTA AMUAHIDI MOURINHO MATAJI BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MITANO CHELSEA

    MSHAMBULIAJI Diego Costa amepania kushinda mataji zaidi baada ya kukamilisha usajili wake Chelsea.
    Mzaliwa huyo wa Brazil, aliiwezesha Atletico Madrid kutwaa taji la La Liga msimu uliopita, na kuifikisha Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya walipofungwa na Real Madrid.
    Jose Mourinho alishindwa kutwaa taji lolote katika msimu wake wa kwanza wa kurejea Stamford Bridge, lakini Costa anajiamini anaweza kumsaidia kutimiza ndoto hizo baada ya kutua magharibi mwa London.  
    Ametua darajani: Diego Costa akemamilisha uhamisho wake Chelsea akitokea Atletico Madrid

    "Nina furaha sana kusaini Chelsea. Kila mtu anajua ni klabu kubwa katika livi ya ushindani sana, na ninavutiwa sana kuanza Ligi Kuu England na kocha babu kubwa na wachezaji wenzangu. Nikiwa nimecheza dhidi ya Chelsea msimu uliopita ninafahamu ubora wa kikosi ninachojiunga nacho,"amesema mchezaji huyo wa Hispania, anayetua Chelsea kwa dau la Pauni 32 kwa Mkataba wa miaka mitano.
    Taarifa ya Chelsea imesema; "Klabu ya Chelsea inayo furaha kutangaza kwamba Diego Costa leo amekamilisha uhamisho wake kutoka Atletico Madrid kwa kusaini Mkataba wa miaka mitano. Atajiunga na kikosi cha kwanza wiki ijayo kwa ajili ya ziara ya Ulaya kujiandaa na msimu," .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIEGO COSTA AMUAHIDI MOURINHO MATAJI BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MITANO CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top