• HABARI MPYA

    Saturday, July 05, 2014

    LIVERPOOL YAKUBALI KUMUUZA SUAREZ PAUNI MILIONI 63 BARCELONA, SASA YASOTEA SAINI YA SANCHEZ

    KLABU za Liverpool na Barcelona zimefikia makubaliano ya biashara ya Luis Suarez jana usiku.
    Kituo cha Televisheni ta Katalunya kimeripoti kwamba ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 63 imekubaliwa na Suarez atasaini Mkataba wa miaka mitano, ambao utamfanya awe mchezaji wa nne kulipwa fedha nyingi baada ya Lionel Messi, Neymar na Andres Iniesta.
    Liverpool wanaendelea na mipango ya kutaka kumsajili Alexis Sanchez wa Barcelona azibe pengo la Suarez.
    Dili limetimia: Luis Suarez sasa yuko njiani kuhamia Barcelona.

    Arsenal inabakia kuwa chaguo la kwanza la Sanchez, lakini Manchester City na United zimeonyesha pia nia ya kuitaka huduma yake sawa na Juventus.  
    Sanchez atasafiri kutoka Santiago, Chile hadi Barcelona nchini Hispania kujadili ofa hizo mezani. Barcelona inatarajiwa kutoa tamko rasmi juu ya Suarez kesho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAKUBALI KUMUUZA SUAREZ PAUNI MILIONI 63 BARCELONA, SASA YASOTEA SAINI YA SANCHEZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top