• HABARI MPYA

    Saturday, August 02, 2014

    EVERTON YASAJILI BEKI DOGO HATARI ANAYEFANANISHWA NA RIO FERDINAND ENZI ZAKE

    KLABU ya Everton imetangaza kumsajili kinda wa umri wa miaka 18, beki Brendan Galloway kutoka MK Dons kwa dau ambalo halikutajwa.
    Mwanasoka huyo wa timu ya taifa ya vijana ya England, amesaini Mkataba wa miaka mitano na kikosi cha Roberto Martinez na ataanzia kuchezea kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21.
    Galloway ameichezea jumla ya mechi 17 Dons msimu uliopita na amekuwa akiitwa 'Rio Ferdinand mpya' kutokana na kufanana naye beki huyo wa zamani wa kimataifa wa England kiuchezaji.
    Rio Ferdinand mpya: Brendan Galloway amesaini mkataba wa miaka mitano na Everton
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EVERTON YASAJILI BEKI DOGO HATARI ANAYEFANANISHWA NA RIO FERDINAND ENZI ZAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top