• HABARI MPYA

    Monday, May 04, 2015

    ALGERIA YAINGIZA TIMU TATU MAKUNDI LIGI YA MABINGWA, EL MERREIKH, AL HILAL NAZO ZOTE ZAFUZU

    ALGERIA imekuwa nchi ya kwanza kuingiza timu tatu katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Entente Setif, USM Alger na Mouloudia El Eulma zote kushinda hatua ya 16 bora.
    Mabingwa watetezi, Setif na Eulma wameshinda kwa penalti dhidi Raja Casablanca ya Morocco na CS Sfaxien ya Tunisia mwishoni mwa wiki.
    Na USMA imesonga mbele baada ya kupangwa na Kaloum ya Guinea mchezo ambao ulihamishiwa Bamako kutoka Conakry kwa sababu ya ugongwa wa Ebola.
    El Merreikh ilianza kwa kuitoa Azam FC Raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 3-2

    Nchi za DRC, Misri na Tunisia zimewahi kuingiza timu mbili katika hiyo miaka ya nyuma. Algeria ilipata nafasi tatu baada ya Setif kutwaa taji hilo mwaka jana na klabu hizo zimejiweka katika mazingira mazuri ya kuweka historia.
    Sudan walikuwa wenye furaha pia baada ya Al Hilal (wameitoa Sanga Balende) na El Merreikh (wameitoa Esperance) kufuzu wakati nafasi nyingine tatu zimekwenda kwa TP Mazembe ya DRC (wameitoa Stade Malien), Smouha ya Misri (wameitoa AC Leopards) na Moghreb Tetouan ya Morocco (wameitoa Al Ahly).
    Ni Setif na Mazembe pekee zimewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa wakati Eulma, Smouha na Tetouan wanashiriki hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALGERIA YAINGIZA TIMU TATU MAKUNDI LIGI YA MABINGWA, EL MERREIKH, AL HILAL NAZO ZOTE ZAFUZU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top