BAO pekee la mshambuliaji Adam Adam dakika ya 34 limeipa Mashujaa FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kwa ushindi huo, Mashujaa inafikisha 18 katika mchezo wa 19 na kusogea nafasi ya 13, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 20 za mechi 18 sasa nafasi ya tisa.
0 comments:
Post a Comment