TIMU ya Arsenal jana iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Bao pekee la Arsenal limefungwa na mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 20 na kwa ushindi huo, The Gunners inafikisha pointi 86 katika mchezo wa 37 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Manchester City ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Manchester United baada ya kupoteza mchezo huo inabaki na pointi zake 54 za mechi 36 nafasi ya nane.
0 comments:
Post a Comment