TIMU ya Geita Gold imelazimishwa sare ya bila mabao na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi 25, ingawa inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, wakati Coastal Union inafikisha pointi 38, nayo inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 27.
0 comments:
Post a Comment