TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars leo imetoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Mali katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo uliotangulia jioni ya leo Sudan Kusini iliichapa Shelisheli 5-1 hapo hapo Azam Complex.
Mechi za kwanza juzi, Mali iliichapa Shelisheli 9-0 na Tanzania iliichapa Sudan Kusini 3-0 hapo hapo Azam Complex.
Mechi zijazo, Tanzania itacheza na Shelisheli na Mali dhidi ya Sudan Kusini.
0 comments:
Post a Comment