TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Bakari Nyundo Shime yamefungwa na washambuliaji, Opah Clement Tukumbuke Sanga wa Beşiktaş ya Uturuki na Aisha Khamis Masaka BK Hacken ya Sweden mawili.
Katika mchezo mwingine uliotangulia jioni ya leo, Mali iliikung’uta Shelisheli 9-0 hapo hapo Azam Complex.
0 comments:
Post a Comment