WENYEJI, Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 56 kwa penalti kufuatia kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari.
Timu hizo zitarudiana Agosti 24 Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali – na mshindi wa michezo hyo ya Raundi ya Awali atakutana na mshindi kati ya JKU na Pyramids ya Mısri kuwania kuingia hatua ya makundi, 16 Bora.
0 comments:
Post a Comment