MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 26 na mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize dakika ya 88 akimalizia pası ya kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki.
Ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga, lakini Kagera Sugar leo inapoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani baada ya kuchapwa 1-0 na Singida Black Stars mwishoni mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment