• HABARI MPYA

    Wednesday, October 10, 2012

    WABABE WA YANGA WAKALIWA KOONI NA JKT KAITABA

    Wachezaji wa Kagera wakiwasalimia wachezaji wa JKT leo Uwanja wa Kaitaba. Picha kwa hisani ya Bukoba Sports.

    Na Prince Akbar, Bukoba
    WABABE wa Yanga, Kagera Sugar jioni hii wamelazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu ya Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
    Sare hiyo imeisaidia JKT kupanda kwa nafasi moja kutoka ya 13 hadi ya 12, juu ya JKT Mgambo ya Tanga, wakati Kagera imelingana kila kitu sasa na Yanga, pointi na wastani wa mabao, zikiwa katika nafasi ya nne na ya tano.
    Sare hii, maana yake Kagera imeshindwa kuendeleza wimbi la ushindi waliloanza nalo juzi, wakiifunga Yanga 1-0, kwa bao pekee la Themi Felix katika dakika ya 67 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
    Felix aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.
    Ligi hiyo, itaendelea kesho kwa mchezo mmoja, utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baina ya wenyeji Toto African na Yanga SC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WABABE WA YANGA WAKALIWA KOONI NA JKT KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top