• HABARI MPYA

    Wednesday, October 10, 2012

    ZEN C NA WENGINE WATANO WAWEKEWA PINGAMIZI UCHAGUZI TWFA

    Zen C; Atatoka kwenye pingamizi nne?

    Na Princess Asia
    MWANDISHI wa Habari Mwandamizi wa magazeti ya serikali, Daily News, Habari Leo na Spoti leo, Zena Chande ‘Zen C’, ni miongoni mwa wagombea sita wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Soka kwa Wanawake Tanzania (TWFA) waliowekewa pingamizi na wadau wa mchezo huo.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY ‘mida hii’ kwamba, Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, wagombea wengine ni Joan Minja anayewania nafasi ya Mwenyekiti ambaye amewekwa pingamizi na wadau sita na Isabellah Kapera ambaye anagombea Uenyekiti amewekewa pingamizi moja.
    Wagombea watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF nao wamewekewa pingamizi akiwemo Zen C, aliyewekewa pingamizi nne, wengine ni Julliet Mndeme (pingamizi sita), na Jasmin Soud mwenye pingamizi tatu, wakati Rahim Maguza anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji amewekewa pingamizi moja.
    Wambura amesema pamoja na pingamizi hizo, wagombea wote wanatakiwa kuhudhuria usaili wakiwa na vyeti vyao halisi vya kitaaluma utakaofanyika Oktoba 12, 13 na 14 mwaka huu kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ZEN C NA WENGINE WATANO WAWEKEWA PINGAMIZI UCHAGUZI TWFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top