Tetesi za J'mosi magazeti Ulaya

AC MILAN YAACHANA NA BALOTELLI

KLABU ya AC Milan imesema kwamba hawana mpango na mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli.
Kevin Strootman
Kevin Strootman.
KLABU ya Manchester United inapiga hesabu za kutoa pauni Milioni 14 kumnasa kiungo wa PSV Eindhoven, Kevin Strootman (pichani juu na kushoto), wakati mustakabali wa Darren Fletcher bado haueleweki.
KLABU ya Manchester United, inaamini iko karibu mno kumsajili kinda mwenye kipaji wa Crewe, mshambuliaji mwenye umri wa miaka 18, Nick Powell kwa dau la pauni Milioni 4.
KLABU ya Manchester City imeambulia patupu katika harakati zake za kumnasa mshambuliaji na Nahodha wa Arsenal, Mholanzi Robin van Persie, kutokana na taarifa kusema kwamba, mshambuliaji huyo hatajiunga na klabu nyingine yoyote ya England.
KLABU ya Fulham inamtolea macho mshambuliaji Huddersfield, Jordan Rhodes kama mbadala wa Clint Dempsey, ambaye amebakiza miezi 12 tu katika mkataba wake Craven Cottage.
KLABU ya West Ham inatumai kufanikiwa kumsajili kipa wa Bolton, Jussi Jaaskelainen ndani ya saa 24 zijazo.
MSHAMBULIAJI WA Poland, Robert Lewandowski, aliyefunga bao la kwanza katika Euro 2012, anawaniwa na Manchester United, kwa mujibu wa kocha wa Poland, Franciszek Smuda.
KOCHA mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers anawapigia hesabu Nicklas Bendtner, Mohamed Diame na Matt Jarvis za kuwasijili katika kikosi cha klabu yake hiyo mpya, yenye maskani yake Anfield.

TETESI ZA EURO 2012...

KOCHA Roy Hodgson anaweza kucheza kamari kwa kumchezesha beki majeruhi John Terry dhidi ya Ufaransa Jumatatu.
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Robin van Persie yuko vema na anajiamini kuelekea mechi ya leo ya timu yake, Uholanzi ikifungua dimba na Denmark.
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa, Louis Saha amesema Euro 2012 ni michuano maalum na lazima isiingiliwe na ubaguzi.

PIGO ARSENAL...

KLABU ya Arsenal, imepata pigo baada ya habari kwamba, beki wake Bacary Sagna, kuvunjika kwake mguu kutamuweka nje ya Uwanja mwanzoni mwa msimu ujao. Habari kamili: Daily Mirror 

JEZI MPYA ZA JUVE NA UJUMBE WA...

JEZI mpya za nyumbani za Juventus zitakuwa na maneno "30 on the pitch", ikiwa ni kukumbushia mataji mawili waliyoponywa huko nyuma.