Mshambuliaji wa Daring Club Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mussa Hassan Mgosi, kulia, akiwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ally Yussuf Tigana kushoto leo jioni mjini Dar es Salaam. Kuna tetesi kwamba, Mgosi ametua Dar es Salaam kusaini Yanga, ingawa mwenyewe alipoulizwa alisema amekuja kwa matatizo ya kifamilia na atarejea DRC baada ya wiki mbili. Inakumbukwa Mgosi alisaini mkataba wa mwaka mmoja DC Motema Pemba, Mei, mwaka jana. Je, ni kweli amekuja kusaini Yanga? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona pazia la usajili Bara litakapofunguliwa rasmi mwezi ujao. |
0 comments:
Post a Comment