![]() |
Bradley akishangilia baada ya pambano |
BINGWA wa dunia uzito wa Welter anayetambuliwa na WBO, Manny
Pacquiao usiku wa kuamkia jana amepoteza taji lake kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa na Mmarekani,
Timothy Bradley kufuatia uwamuzi wa kutatanisha mjini Las Vegas.
Licha ya Pacquiao kupiga ngumi 94 ikiwa ni zaidi ya mpinzani
wake, Mfilipino huyo alishindwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka
saba baada ya majaji wawili kumpa Timothy Bradley pointi 115-113.
Jaji mwingine alitofautiana na wenzake, akimpa ushindi
Pacquiao wa pointi 115-113.
Watazamaji wa pambano hilo hawakuridhika na uamuzi
uliotangazwa na walizomea sana baada ya Bradley kutangazwa mshindi na hilo
limezua uwezekano wa pambano la marudiano baadaye mwaka huu.
"Nilihisi nimeshinda," alisema Bradley, ambaye
hapo kabla alikuwa amechapisha tiketi kabambe za kuonyesha pambano la marudano
kufanyika Novemba 10, mwaka huu.
Bradley aliongezea; "Sidhani ni hodari kama wengi
walivyomsifu. Makonde yake hayakua na nguvu."
Pacquiao alichelewa kuingia ukumbini, lakini alipoingia
alianza raundi ya kwanza kiuzembe uzembe ingawa alirusha ngumi tatu katika
sekundi za mwisho wa raundi.
Hadi kufikia raundi ya tano, Bradley alionekana kuzidiwa
kutokana na maumivu ya jeraha la kidole cha mguu, ikionekana kuwa Pacquiao
anaelekea kupata ushindi wa mteremko.
Kwa upande wa Bradley alifanya vizuri katika raundi tatu za
mwisho, lakini watazamaji hawakuridhika na hilo.
Promota wa masumbwi, Bob Bradley alisema haiaminiki.
Aliongezea kusema kuwa punde baada ya pambano kumalizika, alikwenda kwa Bradley
na akamwambia, “Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, lakini sikuweza kumshinda
mtu huyo.”
Pacquiao mwenyewe alisema hakuweza kuamini matokeo hayo.
Aliongezea kuwa; “Nimejitahidi, lakini naona juhudi zangu hazikutosha. Ngumi
zake hazikunidhuru, mara nyingi ngumi zake ziliishia kwenye mikono yangu,” alisema
Pacquiao.
0 comments:
Post a Comment