Tetesi za J'tatu magazeti Ulaya

BENZEMA AIKATAA MAN UNITED, MANCHESTER CITY BADO WANAYE TU

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Karim Benzema, mwenye umri wa miaka 24, amekataa ofa ya kwenda Manchester United, ambao amedai wanamtaka kwa miaka kadhaa sasa.
WAKATI Karim Benzema akiikataa Man United, wapinzani wao, Manchester City hawajakata tamaa ya kumnasa mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
KLABU ya Newcastle imetoa ofa kwa kiungo mkabaji wa Ajax, Vurnon Anita, mwenye umri wa miaka 23, katika jitihada za kujenga kikosi chao imara cha msimu ujao, ambacho wanataka kiingie Tano Bora katika Ligi Kuu msimu ujao.
KLABU ya Arsenal ipo tayari kumtoa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Morocco, Marouane Chamakh mwenye umri wa miaka 28 aende Montpellier katika sehemu ya dili ya kumpata mshambuliaji Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 25.
KOCHA mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers anaweza kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 22, ambaye mwenyewe amekwishaonyesha nia ya kuondoka Stamford Bridge.
KLABU ya Napoli ya Italia, inataka kumchukua beki wa kati wa Arsenal, Johan Djourou, mwenye umri wa miaka 25, ambaye tayari amekwishavutia ofa ya zaidi ya pauni Milioni 8, kwa mujibu wa wakala wake.

TERRY APEWA MIKOBA LEO EURO 2012 

KOCHA wa England, Roy Hodgson amemuambia John Terry kusimama imara katika mechi yao ya ufunguzi ya Euro 2012 leo dhidi ya Ufaransa.
BEKI wa Ujerumani, Mats Hummels anaamini anaweza kutoa msaada wa kuitupa nje ya mashindano Uholanzi Jumatano usiku.
SHIRIKISHO la Soka Urusi limekata rufaa kwa kitendo cha utovu wa nidhamu cha mashabiki wake kilichofanya waadhibiwe na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), siku wakishinda 4-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech.

BLANC KUMRITHI FERGUSON

KOCHA wa Ufaransa, Laurent Blanc ameibua kwua mtu mwingine anayetajwa kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson katika klabu ya Manchester United.
KOCHA wa kikosi cha England cha Olimpiki, Stuart Pearce amemtema kwenye kikosi chake cha wachezaji 35 alichowasilisha Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere, ingawa Chama cha Soka England bado hakijatoa taarifa rasm kwa umma.
GERRY FRANCIS ATUMA UBANI
NAHODHA wa zamani wa England, Gerry Francis ametuma ujumbe wa kuwataki kila la heri kolcha Roy Hodgson na vijana wake kuelekea mechi yao ya ufunguzi ya Euro 2012 dhidi ya Ufaransa leo.