Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya 

AC MILAN WAIAMBIA MAN CITY; HAMUMPATI NG'O THIAGO SILVA

KOCHA mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers ameionya bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ya Anfield kusahau kabisa mpango wa kumuuza mshambuliaji, Luis Suarez, mwenye umri wa miaka 25.
KOCHA wa AC Milan, Massimiliano Allegri amewataka maini mabingwa wa England, Manchester City akiwaambia kwamba beki Thiago Silva, mwenye umri wa miaka 27, hauzwi ng'o.
Rafael van der Vaart refuses to rule out a move to Schalke
Rafael van der Vaart
KIUNGO Mholanzi wa Tottenham, Rafael van der Vaart, mwenye umri wa miaka 29, ameghairi mpango wa kuhamia Schalke, ili awe karibu na mke wake anayefanya kazi TV Channel ya Ujerumani.
BEKI wa Tottenham, Sebastien Bassong ni mtu anayesaakwa, klabu za Monaco na Rubin Kazan za Urusi zikiwa mstari wa mbele kuwania saini ya kisiki hicho chenye umri wa miaka 25.
MSHAMBULIAJI anayewaniwa na Chelsea, Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, hataondoka Sao Paulo hadi mwaka 2014 mwanzoni. Mpachika mabao huyo tayari imeripotiwa anatakiwa kwa dau la pauni Milioni 30 na The Blues.
KLABU ya Tottenham inataka kubeba wachezaji wawili kwa mpigo West Ham, ambao ni kipa Robert Green, mwenye umri wa miaka 32, na beki James Tomkins, mwenye miaka 23.
KLABU za Wigan na Fulham zote zinamuwania mshambuliaji wa Derby, Theo Robinson, mwenye umri wa miaka 23, ambaye amefunga mabao 12 msimu uliopita.

DESAILLY KUMRITHI BRENDAN

BEKI wa zamani wa Chelsea, Marcel Desailly anatajwa kama mtu anayepewa nafasi kubwa kurithi mikoba ya kocha Brendan Rodgers aliyehama Swansea na kutua Liverpool.
Frank Lampard could represent Team GB at the Olympics
Frank Lampard .
KOCHA Brendan Rodgers, aliyetua Liverpool, amesema lazima kutakuwa na kundi la mashabiki Anfield ambao daima hawatamtaka.
BAADA ya kulazimika kutoka kwenye kikosi cha England cha Euro 2012 kutokana na majeruhi, kiungo wa Chelsea na England, Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 33, anaweza kuitwa kwenye kikosi cha Olimpiki.