• HABARI MPYA

    Tuesday, February 12, 2013

    MALINZI AFYEKWA UCHAGUZI TFF, NYAMLANI SASA MGOMBEA PEKEE URAIS

    Malinzi

    Na Prince Akbar
    KAMATI ya Rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana imemuengua Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), Jamal Malinzi kugombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Taarifa ya TFF jana, imesema kwamba mgombea pekee aliyepitishwa katika nafasi ya Urais, inayoachwa wazi na Leodegar Tenga ni Athumani Nyamlani.
    Nyamlani amepeta kuelekea uchaguzi huo, utakaofanyika Februari 24, mwaka huu kwa sababu pingamizi alilowekewa limetupiliwa mbali.
    Wengine walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi.
    Malinzi aaliwekewa pingamizi Agape Fue, ambaye awali alishindwa na kuamua kukata rufaa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MALINZI AFYEKWA UCHAGUZI TFF, NYAMLANI SASA MGOMBEA PEKEE URAIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top