• HABARI MPYA

    Friday, July 05, 2013

    MOYES ASEMA ROONEY ANABAKI NA HAUZWI...NI BAADA YA MSHAMBULIAJI HUYO KUKUTANA FARAGHA NA SIR FERGUSON

    IMEWEKWA JULAI 5, 2013 SAA 3:43 USIKU
    KOCHA David Moyes amesema kwamba Wayne Rooney hatauzwa na Manchester United na hili ni sawa na pigo lingine kwa Arsenal, ambayo ilikuwa inamtaka mchezaji huyo.
    Kocha huyo mpya wa Old Trafford amekutana na Waandishi wa Habari leo kwa mara ya kwanza tangu athibitishwe kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson, kiasi cha miezi miwili iliyopita na akakutana na maswali kibao kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo wa England.
    Moyes amethibitisha kwamba Rooney – ambaye inafahamika alimuambia Ferguson anataka kuondoka– amebadilisha mawazo yake na amesema atabaki klabuni
    Welcome on board: David Moyes has held his first press conference as Manchester United manager
    Karibu kwenye bodi: David Moyes amefanya Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari kama kocha wa Manchester United
    David Moyes
    David Moyes

    David Moyes
    "Wayne hauzwi," amesema. "Ni mchezaji wa Manchester United na atabakia kuwa mchezaji wa Manchester United,".
    "Tumezungumza mara kadhaa. Vyovyo ilivyotokea kabla, na Wayne tunafanya kazi pamoja sasa. Nimeona nuru katika macho yake, anaonekana mwenye furaha na kama anayekwenda kukita chini. Nasonga mbele kufanya naye kaziI na hatauzwa.
    "Kulikuwa kuna kikao cha faragha baina ya Wayne na Sir Alex. Nasona sasa. Sijui kilichozungumzwa katika kikao chao cha faragha. Kama ninavyosema, nasonga mbele katika kumuweka Wayne Rooney katika kiwango sahihi,"alisema.  
    Tiring: The Rooney saga looks to have come to an end after Moyes said the striker was not for sale
    Yameisha: Sakata la Rooney linaonekana kufikia tamati baada ya Moyes kusema mshambuliaji huyo hatauzwa

    Moyes, mwenye umri wa miaka 50, amejiunga na United kwa Mkataba wa miaka sita baada ya kuitumikia kwa miaka 11 Everton.
    David Moyes
    Getting to know you: Moyes in the Old Trafford dug out
    Moyes akiwa ofisi mpya, Old Trafford anaonekana mwenye furaha
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOYES ASEMA ROONEY ANABAKI NA HAUZWI...NI BAADA YA MSHAMBULIAJI HUYO KUKUTANA FARAGHA NA SIR FERGUSON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top