Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 1, 2013 SAA 4:23 USIKU
BEKI bora wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Kaze Gilbet ametua leo nchini kukamilisha idadi ya wachezaji ya watano wa kigeni wa klabu ya Simba SC msimu mpya.
Beki huyo wa klabu ya Vital’O ya Burundi ametua jioni ya leo na kesho anatarajiwa kusaini Mkataba wa kuichezea klabu hiyo.
Simba SC ilishauriwa na mshambuliaji wake mpya, Amisi Tambwe Mrundi wa Vital’O pia kumsajili beki huyo ili kumaliza tatizo lake la safu ya ulinzi na imefanya hivo.
Simba SC iliwazidi kete wapinzani wao wa jadi, Yanga SC katika kuwania saini ya mfungaji huyo bora ya Afrika Mashariki na Kati, Tambwe majira haya ya joto na faida ya ziada ni kuwashauri kuhusu ujenzi wa safu ya ulinzi.
Simba SC iliamua kuachana na mabeki wengine iliyotaka kuwasajili wa kigeni, Waganda, Assumani Buyinzi na Samuel Ssenkoom kwa ajili ya Gilbert.
Mbali ya Gilbert na Tambwe, wachezaji wengine wa kigeni wanaotarajiwa kuwamo katika kikosi cha Simba SC msimu ujao ni Waganda, kipa Abbel Dhaira, beki Joseph Owino na mshambuliaji, Moses Oloya.
Wachezaji wote wamemalizana na Simba SC isipokuwa Oloya tu, ambaye ameahidi kujiunga na klabu hiyo, baada ya kumaliza Mkataba wake na klabu ya Saigon Xuan Thanh ya Vietnam mwezi huu, Agosti.
Wakati huo huo, Simba SC wanatiwa presha na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC ambao nao inasadikiwa wameingia kwenye vita ya kuwania saini ya mchezaji huyo.

![]() |
Kicheko cha ufanisi; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ana furaha sasa baada ya usajili kwenda vizuri |