• HABARI MPYA

    Tuesday, August 06, 2013

    MAN UNITED CHUPUCHUPU KUCHAPWA SWEDEN, KINDA WA CHILE AINUSURU NA ADHABU

    IMEWEKWA AGOSTI 6, 2013 SAA 4:01 USIKU
    MSHAMBULIAJI chipukizi wa Manchester United, Angelo Henriquez amewanusuru Mashetani hao Wekundu kuzama mbele ya AIK Stockholm kwa bao la dakika ya 68 mjini Stockholm.
    Mshambuliaji huyo wa Chile, ambaye alicheza kwa mkopo Wigan Athletic msimu uliopita, alifunga bao kufuatia jitihada za Wilfried Zaha.
    Kikosi cha David Moyes kilipachikwa bao dakika chache tu baada ya kipindi cha pili lililofungwa na Robin Quaison dakika ya 49.
    Kikosi cha United kilikuwa; Lindegaard/Amos dk46, Rafael, Evans/Smalling dk53, Vidic, Evra, Anderson, Carrick, Giggs/Bebe dk79, Zaha/Welbeck dk78, Van Persie na Nani/Henriquez dk31.
    AIK: Stamatopoulos/Carlgren dk46, Ofori/Owusu dk77, Milosevic/Lorentzson dk46, Backman/Sundberg dk85, Johansson/Karlsson dk46, Bahoui/Lundholm dk59, Borges/Persson dk46, Moro/Saletros dk73, Mutumba/Goitom dk69, Quaison/Kouakou dk59, Igboananike/Kamara dk46.
    Angelo Henriquez
    La kusawazisha: Mshambuliaji Angelo Henriquez ameinusuru Manchester United kuzama mbele ya AIK Stockholm leo
    Wilfried Zaha
    Wilfried Zaha alicheza vyema kabla ya kumpisha Danny Welbeck dakika ya 78
    Anderson
    Nyota wa Manchester United, Anderson akipambana na mchezaji wa AIK, Ibrahim Moro
    Robin Van Persie
    Beki wa zamani wa Blackburn Rovers na Leicester City, Nils-Eric Johansson akisaidiana na mchezaji mwenzake, Niklas Backman kumzuia Robin Van Persie
    Patrice Evra
    Beki wa Manchester United, Patrice Evra akipiga shuti 
    David Moyes
    David Moyes (kushoto), akiwa na Msaidizi wake, Steve Round
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAN UNITED CHUPUCHUPU KUCHAPWA SWEDEN, KINDA WA CHILE AINUSURU NA ADHABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top