Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 6, 2013 SAA 4:31 USIKU
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Cristiano Ronaldo atachuana na mpinzani wake mkuu, Lionel Messi wa Barcelona, zote za Hispania kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya.
Taarifa ya UEFA iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo, imesema kwamba, winga wa Bayern Munich, Franck Ribery ataungana na wakali hao katika orodha ya washindani watatyu wa mwisho katika tuzo hiyo ya msimu wa 2012/13.
Hata huyu? Gareth Bale, anatakiwa kwa dau la Pauni Milioni 85 na Real Madrid, naye hajaingia tatu bora
Inauma: Robin van Persie aliishia 10 bora tu
WALIOINGIA 10 BORA
4) Robert Lewandowski (Poland) – Borussia Dortmund (Pointi 80)
5) Arjen Robben (Uholanzi) – FC Bayern München (55)
6) Thomas Müller (Ujerumani) – FC Bayern München (51)
7) Gareth Bale (WalesL) – Tottenham Hotspur FC (48)
8) Bastian Schweinsteiger (Ujerumani) – FC Bayern München (34)
9) Zlatan Ibrahimović (Sweden) – Paris Saint-Germain FC (27)
10) Robin van Persie (Uhoanzi) – Manchester United FC (24)
Mfaransa huyo aliyetoa mchango mkubwa kwa Bayern kutwaa ubingwa wa Ulaya, anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka nje ya klabu za Barcelona na Real Madrid kuingia fainali ya tuzo hiyo tangu mwaka 2011.
Murgentina, Lionel Messi alishinda tuzo hiyo akifuatiwa na Andres Iniesta, mchezaji mwenzake wa Barcelona mwaka jana.
Messi na mpinzani wake wa Real Madrid, mashambuliaji wa Ureno, Ronaldo wameingia fainali mara mfululizo miaka miwili iliyopita.
Wachezaji wenzake watatu Ribery walioshinda mataji matatu na Bayern msimu uliopita- Thomas Mueller, Arjen Robben na Bastian Schweinsteiger waliingia 10 Bora iliyotangazwa mwezi uliopita.
Mshindi ataamuliwa na jopo la Waandishi wa Habari wa soka kutoka nchi zote wanachama wa UEFA katika uchaguzi wa kura za wazi Agosti 29 wakati wa kutajwa kwa doroo ya Ligi ya Mabingwa mjini Monaco.

Muuwaji: Mshambuliaji wa Dortmund, Robert Lewandowski amekuwa wa nne kwenye orodha
Mchawi wa Winga: Licha ya kufunga bao la ushindi lililoipa Bayern ubingwa wa Ulaya, Arjen Robben amepewa nafasi ya tano
Mtu mwingine wa Munich: Thomas Muller amekuwa wa sita
Bastian Schweinseiger amekuwa wa nne na wa mwisho kwenye orodha, namba nane
Na wa mwisho: Zlatan Ibrahimovic amekuwa wa tisa, mbele ya Robin van Persie