IMEWEKWA AGOSTI 6, 2013 SAA 3:32 USIKU
MSHAMBULIAJI Luis Suarez ametemwa kwenye kikosi cha Liverpool kinachokwenda Valerenga kwa matatizo ya goti.
Mpachika mabao huyo wa Uruguay, ambaye mustakabali wake haueleweki katika klabu hiyo, alitarajiwa kuwamo katika kikosi cha Brendan Rodgers kinachokwenda Norway kesho kwa mchezo wa kirafiki, lakini ameachwa Merseyside.
Alipigwa picha akiondoka Uwanja wa mazoezi wa Liverpool, Melwood leo mchana, wakati wachezaji wengine wakiendelea na mazoezi.
VIDEO Angalia David James: Suarez anahitaji kwenda
Nyuma ya kioo: Luis Suarez, akiondoka mazoezini Jumanne, ameachwa kwenye kikosi cha Liverpool kinachokwenda Norway
Hakuna dalili za Suarez: Brendan Rodgers na Steven Gerrard wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Liverpool
KIKOSI CHA LIVERPOOL KITAKACHOMENYANA NA VALARENGA
Jones, Enrique, Toure, Alberto, Gerrard, Aspas, Coutinho, Assaidi, Henderson, Coates, Downing, Spearing, Lucas, Mignolet, Allen, Borini, Sterling, Kelly, Flanagan, Ibe, Wisdom.
Suarez atakwenda kufanyiwa vipimo ili kujua uzito wa maumivu yake kama ataweza kusafiri kwenda Dublin Ijumaa kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Liverpool wa kujipima dhidi ya Celtic Uwanja wa Aviva.
Tangu amerejea kutoka mapumziko yake ya majira haya joto, Suarez amecheza akitokea benchi katika mechi dhidi ya Melbourne Victory, Thailand na Olympiakos Jumamosi iliyopita, huku akizungumziwa sana kuondoka Anfield.
Hana furaha: Suarez anatarajiwa kuondoka Liverpool, na Arsenal iko mstari wa mbeke kumsajili
Benchi: Brendan Rodgers anakwenda na timu yake Oslo kumenyana na Valarenga bila Suarez
Liverpool imeendelea na msimamo wake wa kutotaka kumuuza Suarez, ingawa anahusishwa kwa kiasi kikubwa na Arsenal.
Timu ya Arsene Wenger imekwishatoa ofa mbili - moja ya Pauni Milioni 35, nyingine ya Pauni 40,000,001 - ambazo zote zimepigwa chini.
Kukosekana kwake kesho hakutavuruga mipango ya Rodgers kuelekea msimu mpya, kwani Suarez atakosa mechi sita, akitumia adhabu yake iliyosalia kutokana na kumng'ata Branislav Ivanovic.
Rodgers amemchukua pia Daniel Sturridge aliyerejea baada ya kupona kifundo cha mguu.
Tegemeo: Itakuwa pigo kubwa kwa Liverpool ikiwa Suarez ataondoka
Kocha wake mpya? Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekwishatoa ofa mbili zilizopigwa chini Liverpool