IMEWEKWA AGOSTI 6, 2013 SAA 1:55 USIKU
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Robin van Persie amesherehekea miaka 30 ya kuzaliwa kwake leo, na mpishi wa klabu alitoa mchango wake.
United imetweet picha ya keki iliyotengenezwa na mpishi wa klabu kwa ajili ya Van Persie, ikiwa na ujumbe usemao; 'Happy Birthday' katika lugha ya Kiholanzi.
Mapema, klabu pia ilichangia bago la 'RVP' kwa heshima ya mfun gaji wao huyo bora msimu uliopita kutimiza miaka 30.
Van Persie alifunga mabao 31 United msimu uliopita baada ya kuhamia akitokea Arsenal.
Kwako, Robin: Mpishi wa United ameonyesha keki aliyomtengenezea Robin van Persie, ikisema 'Happy Birthday' Kiholanzi
Furahia kuzaliwa: Manchester United imetweet picha hii ya Van Persie akitimiza miaka 30 Jumanne
Matawi ya juu: Van Persie alikuwa mfungaji bora wa United msimu uliopita kwa mabao 31
Wakati huo huo, wakati United ikijiandaa na mchezo wake ujao na Stockholm, Nani na Bebe wanatarajiwa kuukosa mchezo huo baada ya kucheza mpira wa meza.
Mabingwa wa England wapo Sweden kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya AIK Fotboll leo usiku, na Nani na Bebe walikuwa wakicheza mpira wa meza katika hoteli ambayo timu imefikia Stockholm.
Kikosi cha David Moyes kimeshinda mechi mbili tu katika mechi tano za kujiandaa na msimu kwenye ziara yake ya Asia na Australia.
United ilifungwa 1-0 na Singha All Stars Julai 13 na wakafungwa tena Yokohama F-Marinos 3-2.
Kichwa kwa kichwa; Nani (kushoto) akicheza na mchezaji mwenzake Bebe (kulia) mpira wa meza
Lakini ushindi wa 5-1 dhidi ya A-League All Stars na 5-2 dhidi ya Kitchee ulirejesha matumaini kwamba United bado ina safu ya nguvu ya ushambuliaji iliyowawezesha kuweka rekodi ya kutwaa taji la 20 msimu uliopita.
Vijana wa Moyes walihitimisha mechi zao za kujiandaa na msimu kwa mechi ya kumuaga Rio Ferdinand usiku wa Ijumaa Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Sevilla kabla ya kumenyana na Wigan katika mechi ya Ngao ya Jamii Jumapili.
Kampeni ya kutetea taji lao inaanza Jumamosi, Agosti 17 na Swansea ugenini.