• HABARI MPYA

    Sunday, October 06, 2013

    PAMBANO LA RUVU, SIMBA LAINGIZA MILIONI 75


    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA OKTOBA 6, 2013 SAA 6:46 MCHANA
    MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Simba lililochezwa jana (Oktoba 5 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 75,692,000.
    Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 43 la VPL msimu wa 2013/2014 lililomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 13,395.
    Haroun Chanongo akipasua, kushoto ni Henry Joseph akiwa tayari kutoa msaada

    Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 17,983,902.31 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,546,237.29.
    Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,144,357.11, tiketi sh. 3,183,382, gharama za mechi sh. 5,486,614.26, Kamati ya Ligi sh. 5,486,614.26, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,743,307.13, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,066,841.66 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,066,841.66.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PAMBANO LA RUVU, SIMBA LAINGIZA MILIONI 75 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top