Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA OKTOBA 3, 2013 SAA 2:03 ASUBUHI
SIMBA SC imewasilisha malalamiko Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ya madai ya dola za Kimarekani 300,000 za mauzo ya mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku kwamba, wametuma barua pepe FIFA kufungua rasmi malalamiko ya madai ya fedha hizo, baada ya E.S.S. kushindwa kulipa kama ilivyoahidi Septemba 30, mwaka huu.
“Kwa hiyo tunasubiri majibu yao (FIFA), kwa sababu hata wao wanajua kwamba usajili wa yule mchezaji ulifanyika bila malipo, kwa hiyo tutakapopata majibu yao tutakuwa na cha kuzungumza,”alisema Poppe.
Okwi, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda ambaye hivi karibuni alikuja kutembea Dar es Salaam, amesusa kurejea Tunisia kutokana na madai ya klabu hiyo kushindwa kumlipa mishahara kwa miezi mitatu.
Okwi amekaririwa akisema kwamba tayari kesi yake ameifikisha pia FIFA, wakati Etoile nayo imekaririwa kudai imemshitaki mchezaji huyo FIFA pia kwa kushindwa kuripoti kazini kwa muda mrefu sasa, baada ya ruhusa ya kwenda kujiunga na timu yake ya taifa zaidi ya miezi miwili iliyopita.
Baada ya kumnunua mchezaji huyo Januari mwaka huu, Etoile iliahidi kutuma fedha za manunuzi yake mjini Dar es Salaam, lakini siku zilikatika hadi katikati ya mwaka, uongozi wa Simba ulipolazimika kwenda Tunisi kufuatilia fedha hizo.
Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Hans Poppe aliongozana na Katibu wa klabu, Mwanasheria, Evodius Mtawala hadi Tunis na wakiwa huko, klabu hiyo iliahidi kulipa fedha hizo Septemba 30, lakini leo Oktoba 3 bado haijfanya hivyo.
Katikati ya ahadi hiyo, Okwi naye akasusa kwa madai ya kutolipwa mishahara- jambo ambalo linazidi kuiweka pagumu biashara hiyo, ingawa kwa mujibu wa sheria, Etoile wanatakiwa kuilipa Simba SC fedha zake kisha kuendelea na kesi yao na mchezaji huyo.
Mkataba ambao Simba SC ilisaini na Etoile kuhusu Okwi, mbali na kulipwa dola 300,000 pia una kipengele cha atakapouzwa timu yoyote, Wekundu wa Msimbazi wapewe sehemu ya fedha.

![]() |
Kesi FIFA; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba SC, Zacharia Hans Poppe |