• HABARI MPYA

    Thursday, October 03, 2013

    SAMATTA, ULIMWENGU WAPAA NA MAZEMBE LEO KUFUATA TIKETI YA FAINALI AFRIKA

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA OKTOBA 3, 2013 SAA 3:05 ASUBUHI
    TOUT Puissant Mazembe ya DRC inayojivunia washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu inaondoka leo mchana Accra kwenda Mali tayari kwa mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya wenyeji Stade Malien Jumamosi mjini Bamako. 
    Baada ya wiki moja ya maandalizi na mazoezi ya mara mbili kwa siku Uwanja wa Lizzy Sports Complex kikosi cha mabingwa hao mara nne Afrika kinaondoka leo kwenda Bamako, kikiwa vizuri kabisa.
    Mazoezi ya nguvu; Ulimwengu juu na Samatta chini wakijifua

    Nahodha wa Mazembe, Tresor Mputu amesifu kambi ilikuwa nzuri na kwa ujumla yeye na wachezaji wenzake wako tayari kabisa kwa vita ya kugombea tiketi ya fainali ya Kombe la Shirishiko.
    “Mechi itakuwa ngumu, lakini tumejiandaa vizuri, tulikuwa tunafanya mazoezi kila siku, ya ufundi na nguvu na kwa ujumla tuko vizuri kuelekea mchezo huo,”alisema Mputu, ambaye kwa sasa yeye na akina Ulimwengu na Samatta ndio tegemeo la mabao la Mazembe.
    Amesema lengo lao lao ni kutwaa Kombe la Shirikisho ili kuwapa raha mashabiki wao, baada ya kukosa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Kiongozi; Nahodha wa TPM, Tresor Mputu ana matumaini ya ushindi Bamako

    Katika kambi yao ya Accra, wapachika mabao wa Tanzania, Samatta na Ulimwengu wameonekana wako fiti kwa kiasi kikubwa kuelekea mchezo huo wa Jumamosi.
    Mbali na mechi hiyo ya Bamako, Nusu Fainali nyingine itazikutanisha timu za Tunisia tupu, CA Bizertin na CS Sfaxien ambako mshindi wa hapo atamenyana na mshindi wa jumla kati ya Stade Malien na TP Mazembe.
    Mechi za marudiano zitachezwa Jumamosi ya Oktoba 19, Mazemebe wakimalizia nyumbani Lubumbashi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SAMATTA, ULIMWENGU WAPAA NA MAZEMBE LEO KUFUATA TIKETI YA FAINALI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top