• HABARI MPYA

    Thursday, October 03, 2013

    NYUMBA YA NIYONZIMA YAUNGUA MAGOMENI MAKUTI

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA OKTOBA 3, 2013 SAA 3:50 ASUBUHI
    NYUMBA anayoishi kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima, maeneo ya Magomeni Makuti, Dar es Salaam imeungua moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha hasara ya vitu kadhaa. 
    Habari zilizoifikia BIN ZUBEIRY zimesema kwamba nyumba hiyo anayopanga mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda, imeungua zaidi eneo la sebuleni na fenicha zote, Teleisheni na Redio zimeteketea kwa moto.
    Pole rafiki; Nyumba anayoishi kiungo Haruna Niyonzima wa Yanga SC imeungua moto

    Janga hilo lilitokea wakati mchezaji mwenyewe akiwa ndani ya nyumba yake na kama si jitihada za majirani kujitokeza kumsaidia kuzma moto huo, athari zingekuwa kubwa.
    Imeelezwa nyumba hiyo ina wapangaji wawili na upande ulioathirika kwa moto ni ambao anasihi mchezaji huyo tu.
    Hasara; Niyonzima akiwa nyumbani kwake baada ajali ya moto
    Jitihada za kumpata Haruna mwenyewe haraka kuzungumzia suala hilo hazijafanikiwa na zinadenelea, wakati Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto alisema amesikia taarifa hizo ila anasubiri kupata uhakika kamili kutoka kwa mchezaji mwenyewe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NYUMBA YA NIYONZIMA YAUNGUA MAGOMENI MAKUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top