IMEWEKWA OKTOBA 6, 2013 SAA 11:46 ALFAJIRI
BAADA ya kimya cha muda mrefu, hatimaye wiki hii Yanga SC imeibuka tena na hadithi ya ujenzi wa Uwanja wake, ikitoa taarifa ya sababu ya kukwama kwa ahadi hiyo.
Nitawakumbusha taarifa hiyo; “Leo tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana
Mara ya mwisho tuliongea ama kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabidhi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKIACHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO, lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.
Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:
• Kupata na kuwa na eneo la kutosheleza malengo ya mradi
• Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na mkandarasi mzuri wa mradi
• Kupata na kutenga fedha za kukamilisha usanifu na ujenzi wa mradi
Kwa upande wa BCEG wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.
Kutokana na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na mioundombinu ifuatayo:-
1. Uwanja wa mpira wenye viti 40,000
2. Hostel ya wachezaji na football academy ya vijana
3. Viwanja vya mazoezi
4. Uwanja wa kutosha kuegesha magari
5. Hoteli na sehemu ya makazi
6. Ukumbi wa mikutano
7. Sehemu ya maofisi, benki, zahanati (sports clinic)
8. Maduka, supermarket na sinema
9. Sehemu za kubarizi, kupumzikia (Recreational and Open spaces)
Mara baada ya azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani City” na kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende maeneo ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili litaboresha mandhari nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na miundombinu. Hii itahusu pamoja na mambo mengine ujazaji udongo (tuta kubwa), upandaji miti, bustani za kubarizi, kuboresha mifereji ya majitaka na kudhibiti mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia sura ya kibiashara na kitalii.
Ili kukamilisha azma ya kuwa na Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu yote hiyo, Uongozi ulipeleka maombi ya eneo la nyongeza Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa barua zenye kumbukumbu namba YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba 2012, na mpaka sasa bado maombi yetu hayajajibiwa.
Mwezi wa saba, Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Klabu ya Yanga ina kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani. Kiwanja hiki kina hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika eneo hilo, klabu ilifanikiwa kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na Jengo la klabu la ghorofa tatu. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili mkubwa sana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) na michango ya wanachama na wapenzi wa klabu ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa haba na haba hujaza kibaba.
Ndugu Wandishi wa habari kwa kifupi tumefikia hapo, zoezi la kutoa maoni yetu kuhusu michoro ya usanifu wa awali na kuingia rasmi mkataba wa ujenzi na BCEG limesimama, likisubiri majibu ya nyongeza la eneo. Ni matumaini yetu zoezi hili litakamilika hivi karibuni na kuendelea na mradi”.
Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga SC, Francis Mponjoli Kifukwe ndiye aliyetoa taarifa hiyo Septemba 30, mwaka huu.
Baadaye, Serikali ikawajibu ikisema kwamba Yanga haiwezi kupewa eneo la ziada kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wake wa kisasa wa soka. Ofisa Habari wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rehema Isengo alisema tayari eneo la Jangwani liko katika mipango ya maendeleo.
Rehema alisema katika mazungumzo ya awali kati ya Wizara na Manispaa, tayari eneo la Jangwani liko kwenye mradi wa kujengwa City Garden, hivyo Yanga haiwezi kupewa eneo hilo.
Alisema Yanga ilishapewa majibu hayo kupitia ofisi ya Mipango Miji na kuongeza kuwa, Wizara haihusiki na ugawaji wa viwanja kwa vile suala hilo lipo chini ya Halmashauri.
Alisema kazi ya Wizara ni kupitia faili lililowasilishwa kabla ya kutia saini. Mbali na hilo, Rehema alisema Yanga inadaiwa deni la kodi ya Ardhi tangu mwaka 1997 hivyo ameitaka kulilipa mara moja.
"Yanga siyo walipaji wazuri wa kodi, wanadaiwa kodi tangu 1997, wameshapewa maelezo wafuatilie na kulipa kodi hiyo,"aliongeza. Ofisa Habari huyo aliweka wazi kuwa, athari inazoweza kupata Yanga endapo itashindwa kulipa deni hilo ni kunadiwa kwa mali zake au kupelekwa mahakamani.
Lakini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadick akaingilia suala hilo kwa lengo la kuwasaidia Yanga SC akisema kwamba kuna watu walivamia kiwanja chao pale Jangwani na kujenga, hivyo wanatakiwa kuhama ili klabu hiyo ipate eneo zaidi kwa ajili ya kutekeleza mradi wake.
Ukweli ni kwamba, hapa kuna dalili za mgogoro ambao unaweza kuepukwa- Yanga kulazimisha kujenga Uwanja pale Jangwani, hata ikibidi kwa kubomoa nyumba za wakazi wa eneo hilo waliovamia ni jambo ambalo linaweza kusababisha ‘balaa’.
Mgogoro wa Serikali na wakazi wa Jangwani, ni ambao unajulikana kwa muda mrefu juu ya ugumu wake, tangu Alhaj Ally Hassan Mwinyi bado Rais wa Jamhuri ya Muungano wetu- wazi kutaka kuufufua sasa ili tu kuwaridhisha Yanga SC kuna hatari inakaribishwa.
Inafahamika, eneo lile Yanga walipewa na Serikali bure, hawakununua na sheria za Ardhi, mtu au taasisi anapopewa eneo kwa ajili uwekezaji anapewa na muda maalum wa uendelezaji, anaposhindwa, Serikali inaweza kumgawia mtu mwingine.
Yanga SC baada ya kupewa eneo kubwa, wakajenga uzio katika eneo ambalo waliona litawatosha kwa mahitaji yao ya kujenga Uwanja uliopo sasa na jengo, na eneo lililobaki wakashindwa kuliendeleza na pale Jangwani ni katikati ya mji, walitegemea nini?
Kumbukumbu zinaonyesha mapema tu mwaka 1972 tayari Yanga SC walikwishasimamisha jengo lao na leo hii ni zaidi ya miaka 40, hii kesi inaweza kuamuliwa vipi? Ndiyo maana ninasema kuna janga linakaribishwa hapa, kwa sababu baadhi wa wakazi ambao wanadaiwa walivamia eneo hilo, walifuata taratibu za kisheria kupata maeneo hayo.
Ukweli ni kwamba, haya yanayoibuka sasa ni kwa sababu Yanga SC wameamka na wamejua thamani ya ardhi na kwa kuwa pia wana mahitaji nayo kwa wakati huu. Lakini hiyo haiwezi kufuta makosa yao yaliyowasababisha wakapoteza sehemu kubwa ya ardhi yao pale Jangwani.
Kwa kuwa Yanga SC wanahitaji Uwanja, kwa sababu kwa sasa hawana hata Uwanja wa mazoezi- ni vyema wakafanya kile ambacho kinawezekana bila ya kumuathiri mtu, au watu wengine. Uwanja wenye kukidhi mahitaji yasiyo makubwa unawezekana kujengwa ndani ya eneo ambalo wanamiliki Yanga SC kwa sasa mbali na lile ambalo wanadai limevamiwa.
Na kama Yanga SC wanahitaji kujenga Uwanja ambao kama ambao ameuelezea Kifukwe, Dar es Salaam bado kubwa, wanaweza kupata eneo lingine nje ya mji wakatimiza ndoto zao. Na hakuna shaka yoyote, kwa sababu Yanga ni klabu kubwa na popote itakapoweka maskani watu wataifuata tu, kwa sababu wanaipenda.
Jambo bora kwa sasa ni Yanga SC kufanya kile kinachowezekana bila ya kumuathiri mtu, au watu wengine, au kusababisha uvunjifu wa amani. Jumapili njema.