IMEWEKWA IOKTOBA 6, 2013 SAA 12:00 ASUBUHI
BONDIA Wladimir Klitschko ameendelea kutawala ndondi za uzito wa juu baaya usiku wa kuamkia leo kuvunja rekodi ya kutopigwa ya Alexander Povetkin mjini Moscow.
Mdogo wa ndugu wawili wanaotawala ndondi za uzito wa juu kwa zaidi ya miaka saba sasa, alitarajiwa kukutana na upinzani mkali ulingoni mbele ya mshindi huyo wa zamani wa Medali ya Dhahabu ya Olimpiki.
Lakini mbabe huyo mwenye umri wa miaka 37 alipata ushindi mwepesi, akimuangusha chini Povetkin mara nne na kutetea mataji yake ya WBO, IBO, IBF na WBA.
Bado bingwa: Wladimir Klitschko akishangilia baada ya kumpiga Alexander Povetkin
Klitschko, ambaye alilipwa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 17 (Pauni Milion 11) hilo likiwa pambano la pili la 'utajiri mkubwa' kwa mabondia wa uzito wa juu baada ya lile la Mike Tyson alilopigwa na Lennox Lewis, alityawala pambano tangu kengele ya kwanza, akitumia mikono yake mirefu kumnyayasa Povetkin.
Mrusi hiyo alifondoshwa mara moja katika Raundi ya pili na mara tatu katika raundi ya saba, kabla ya Klitschko kukatwa pointi kwa kumshika mpinzani wake.
Hiyo haikusaidia kwa Povetkin kushinda pambano hilo, kushindwa kwa kwa pointi 119-104 za majaji wote.
Chali babake: Wladimir Klitschko alimuangusha chini Alexander Povetkin mara nne
Alexander Povetkin akihesabiwa na refa baada ya kuinuka
"Alexander ni mpiganaji na ilikuwa vigumu kwake, kwa sababu nilimuumiza. Lakini aliendelea, kwa sababu ana moyo mkubwa," alisema Klitschko baada ya pambano.
"Nilitaka nimalize pambano mapema. Nilitaka kumpa ngumi moja kubwa na nafikiri nilifanya vizuri.'
Kichapo cha mbwa mwizi: Klitschko akimpa makonde Povetkin ambaye alikuwa hajawahi kupigwa
Anajikokota; Povetkin akijikokota kuinuka ili kuendelea na pambano baada ya kudondoshwa na masumbwi ya Klitschko.
"Bado nafanya mazoezi magumu ili niwe na nguvu zaidi," alisema. "Wakati mwingine haifanyi kazi kama ninavyotaka. Niliweka kila kitu pale.
"Siwezi kusalimu amri. Napigana mpaka mwisho kabisa. Klitschko alikuwa ana nguvu, ni bora duniani kwa wakati huu.'
Maji marefu: Povetkin alijitahidi kupambana ulingoni, lakini ukwi ni kwamba alikutana na mtu mkali ulingoni
Bado bingwa: Klitschko ametetea ubingwa wake wa uzito wa juu kwa kumtwanga Povetkin mjini Moscow